Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, kushoto akimpatia hati ya kiwanja cha Vikuruti, mteja wao Ibrahim Yusuph Ismail, nyumbani kwao Kariakoo jijini Dar es Salaam, leo mchana. Kwa wiki hii tu Bayport imeamua kuwapelekea hati za viwanja wateja wao katika maeneo yao ya makazi na maofisini kwao.
Hati za viwanja vya Bayport zatolewa kwa mtindo wa aina yake
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, wateja wa Bayport
waliojipatia viwanja vya Bayport vilivyopo Vikuruti, Mlandizi, wilayani Kibaha
mkoani Pwani wameendelea kupewa hati zao, huku safari hii wakipewa hati kwenye
maeneo wanayopatikana ikiwamo majumbani na maofisini.
Hatua za kuwapelekea hati hizo wateja wao ni kitendo cha
kuthamini uwapo wa wateja wao wanaoendelea kuiamini Bayport Financial Services
katika bidhaa zake za mikopo ya fedha, bila kusahau huduma ya mikopo ya viwanja
vyenye hati inayotolewa na taasisi hiyo, kwa kushirikiana na wadau wa ardhi
walioingia mikataba na Halmashauri unapopatikana mradi wa viwanja kwa ajili ya
watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi, wajasiriamali na Watanzania
kwa ujumla.
Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabiti Mndeme, kushoto akizungumza jambo wakati anamkabidhi hati yake ya kiwanja mteja wao Neema Jameson Nawita, jijini Dar es Salaam leo mchana.
Akizungumza wakati wa kutoa hati kwa wateja watatu leo jijini Dares Salaam, Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, alisema jambo kubwa la miradi ya viwanja kwenye taasisi yao ni kuona weteja wao wanapata hati ili kuweka ubora wa huduma zao, ikiwa ni sehemu muafaka ya kufuta migogoro ya ardhi kwa kununua viwanja vyenye hati. Alisema kwa wiki mbili mfululizo wamekuwa wakiendelea kutoa hati kwa wateja wao, huku kwa wiki hii tu, taasisi hiyo ikifika mbali kwa kujenga imani na kwenda sambamba na wateja hao, wakaona umuhimu wa kuwathamini na kuwataka wachague maeneo wanayoona wanaweza kupokea hati zao, iwe ni maofisini kwao au kwenye maeneo ya makazi.
Mteja wa Bayport na mkazi wa jiji la Dar es Salaam, Neema Jameson Nawita, kulia akipokea hati yake ya kiwanja cha Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, aliyokabidhiwa leo na Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services.
Mteja wa Bayport na mkazi wa jiji la Dar es Salaam, Neema Jameson Nawita,kulia akizungumza na waandishi baada ya kukabidhiwa hati yake ya kiwanja cha Vikuruti, Mlandizi,wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Kushoto ni Thabit Mndeme, Meneja Biashara wa Bayport Financial Services.
Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, kushoto akimkabidhi hati ya kiwanja cha Vikuruti, Mlandizi, wilayani Kibaha mkoani Pwani mteja wao Hassan Omary Hamis, jijini Dar es Salaam, leo mchana.
Sign up here with your email