Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora imeahirisha kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi Jimbo la Kigoma Kusini iliyofunguliwa na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, David Kafulila, kupitia chama cha NCCR-Mageuzi akipinga ushindi wa Mbunge Hasna Mwilima, wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kesi hiyo iliahirishwa jana na Jaji wa mahakama hiyo, Ferdinand Wambali, baada ya Wakili wa kujitegemea, Profesa Abdallah Safari, anamtetea mlalamikaji kuomba mahakama hiyo impatie saa 48 ili akamilishe hati za kiapo za mashahidi wake watano na baada ya hapo mahakama ipange tarehe nyingine ya kutajwa kwa ajili ya kuanza kusikiliza.
Jaji Wambali alikubaliana na ombi hilo na kusema hati za mashahidi zipelekwe kwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, Shanmillah Sanwatt, zikiwa zimefungwa kwenye bahasha Machi 18, mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kigoma.
Sign up here with your email