FILAMU ZETU HAZIVUTII KWASABABU MAADILI YANATUBANA. Richie amesema moja ya sababu kubwa ya filamu za kibongo kutovutia ni maadili yanayowabana kuigiza uhalisia wa kile kinachotokea kwenye jamii. Akizungumza na ,Richie amefafanua kuwa kuna maneno ambayo kiuhalisia yanatumika mtaani hasa kwenye sehemu za vurugu au magenge ya wahuni,lakini ukiyatumia kwenye filamu katika #Scene zinazohusu maeneo kama hayo Filamu hiyo haitaruhusiwa kutolewa kwa kisingizio haina maadili. Amelalamikia issue hiyo akisema inafanya wao kushindwa kushindana kimataifa kwasababu nchi nyingine wameruhusiwa kufanya hivyo. Ametolea mfano wa filamu maarufu nchini Kenya 'NAIROBI HALF LIFE"ambayo ilitumia maneno halisi kulingana na sehemu husika na ikaitangaza Kenya kote duniani.
Sign up here with your email