
Waziri mkuu wa Tanzania Kasim Majaliwa amewataka mawaziri kuhakikisha wanajiepusha na vitendo vya rushwa na ufisadi kwa kufuata sheria ya maadili ya viongozi wa umma ili kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Akifungua mafunzo ya maadili ya utumishi wa umma kwa mawaziri leo Ikulu jijini Dar ee salaam Mhe. Majaliwa amesema kumekuwa na ukiukwaji wa maadili ya viongozi wa umma nchini na kuongeza malalamiko kwa wananchi yanayohusu vitendo vya rushwa katika taasis za serikali na kuzorotesha ufanisi wa serikali katika kutoa huduma kwa wananchi.
Katika mafunzo hayo yanayowashirikisha mawaziri 24, Waziri Mkuu Majaliwa amesema viongozi wa serikali wanao wajibu wa kusimamia rasilimali za umma kwa kufuata sheria za maadili ya umma.
Awali akimkaribisha waziri mkuu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora The Angela Kairuki amesema atahakikisha watumishi wa umma wanazingatia utawala bora kwa kufuata maadili ya utumishi wa umma.
Kamishna wa sekretarieti ya maadili ya utumishi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda amesema uchache wa watumishi na ukosefu wa fedha umesababisha kushindwa kuhakiki mali za watumishi wa umma kwa mwaka wa tatu sasa hali inayochangia kuongezeka kwa ubadhirifu kwa viongozi wa serikali.
Sign up here with your email