Leo tarehe 6 Februari ni Siku ya Kupinga Ukeketaji dhidi ya Wanawake na Watoto wa Kike Duniani.
Kwa mujibu wa Takwimu za Demografia na Afya Tanzania (Tanzania Demographic and Health Survey - TDHS 2010) asilimia 15 ya wanawake Tanzania wamefanyiwa Ukeketaji. Ukeketaji ni ukatili dhidi ya watoto wa kike na wanawake. Na ni kosa la jinai. Madhara ya ukeketaji ni pamoja na vifo, vilema na maradhi kama fistula na mengineyo.
Serikali itaendelea kukemea na kupambana na vitendo hivi katika jamii zetu, katika nchi yetu. Tutaongeza jitihada za kutoa elimu kwa jamii sambamba na kuwachukulia hatua wote wanaojihusisha na vitendo hivi. Nawataka Maafisa Maendeleo ya Jamii katika Mikoa, Wilaya na Kata kuongeza nguvu ktk kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa lengo la kuhakikisha wazazi/walezi, mangariba na wote wanaojihusisha na vitendo vya Ukeketaji wanafikishwa ktk vyombo vya dola ili sheria ichukue mkondo wake.
Ninapenda kutoa wito kwa kila mmoja wetu kushiriki katika mapambano haya hasa katika kutoa taarifa na ushahidi Mahakamani.
Nitoe shukrani zangu za dhati kwa mashirika yasiyo ya Kiserikali na wadau wote wanaopinga ukeketaji Tanzania.
Pamoja Tunaweza Tokomeza Ukeketaji Tanzania!
Sign up here with your email