WATU 14 WAKUTWA WAMEJIFICHA NDANI YA KISIMA. - Rhevan Media

WATU 14 WAKUTWA WAMEJIFICHA NDANI YA KISIMA.

Embedded image permalink

Idara ya uhamiaji mkoani Kagera imetoa muda wa siku kumi na nne kwa wahamiaji haramu na wageni wanaofanya kazi katika mkoa huo bila kuwa na vibali ambao wamejificha kwenye baadhi ya visiwa vilivyoko ndani ya ziwa Victoria ambao kwa kukimbia msako maalumu unaofanywa na idara hiyo kwa kushirikiana na idara ya kazi wenye lengo la kuwabaini wageni wanaoishi na kufanya kazi hapa nchini kinyume na taratibu kujisalimisha mara moja. 
Akizungumza ofisini kwake leo afisa wa idara ya uhamiaji mkoani Kagera, Abdallah Towo ambaye ni kamishina msaidizi mwandamizi amesema msako unaofanywa na idara ya uhamiaji wenye lengo la kuwabaini wahamiaji haramu na wanaofanya kazi bila vibali kuwa ni endelevu hivyo katika kipindi hicho kilichotolewa kwa wale wote waliojificha wajitokeze kabla ya kufanyika shughuli ya kuwasaka itakayovihusisha vyombo vyote vya dola. 
 
Akizungumzia juu ya msako unaoendeshwa na idara hiyo katika maeneo mbalimbali yaliyoko mkoani Kagera ya kuwabaini wahamiaji haramu na wanaofanya kazi bila vibali, afisa huyo amesema kwa mwezi januari idara hiyo ilifanya misako ya kushtukiza katika taasisi mbalimbali kumi na tano na kuwabaini wageni tisini na saba wanaofanya kazi katika taasisi hizo kati ya wageni hao watano kwalikutwa hawana vibali vya kufanya kazi na kuishi nchini, pia iliwanasa wahamiaji haramu tisini na mbili ambao walifikishwa mahakamani na wengine kufukuzwa nchini huku wanaowaingiza nchini wakitozwa faini.
 
Kwa upande wake, afisa kazi mfawidhi katika mkoa wa Kagera, Samwel Mgila amewataka waajili katika mkoa wa Kagera hasa wanaomiliki shule binafsi za sekondari na za msingi kufuata taratibu na kanuni katika suala zima la kutoa ajira kwa wageni toka nje ya nchi. 
 
Mkoa wa Kagera ni moja ya mikoa inayokabiliwa na wimbi kubwa la wahamiaji haramu mkoa huo unakadiliwa kuwa na wahamiaji haramu zaidi ya elfu therathini na tisa toka katika nchi mbalimbali zinazopakana na mkoa huo, wahamiaji haramu walio wengi wanaishi maeneo ya vijijini.