
Balozi mpya wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo nchini Tanzania JEAN MUTAMBA amepongeza kasi ya utendaji kazi ya Rais JOHN MAGUFULI na kuahidi kushirikiana nae sanjari na kutanua wigo wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili. Balozi Mutamba amebainisha hayo baada ya kukabidhi nakala za utambulisho Ikulu na kisha kupokelewa katika ofisi za ubalozi wa Kongo hapa nchini. Balozi MUTAMBA pia amekutana na wafanyabiashara wa Kongo na baadhi ya raia wa Kongo waishio nchini Tanzania, na kuahidi kudumisha ushirikiano. Nae Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wakongo waishio Tanzania EMMANUEL MBOSWA akamuomba balozi huyo kusaidia kupunguza masharti ya upatikanaji wa vibali vya kuishi hapa nchini.
Sign up here with your email