
Baada ya jana kuugomea uongozi wao kwa madai ya kucheleweshea mishahara yao ya miezi mitatu - Wachezaji wa Coastal Union leo walilipwa kila mmoja mshahara wa mwezi mmoja na muda mfupi baadae wakaingia uwanjani kucheza dhidi ya Mtibwa katika michuano ya kombe la FA. Matokeo ya mchezo huo, Coastal wameshinda 1-0 katika uwanja wa Mkwakwani - Tanga.
Sign up here with your email