
Mkurugenzi Mkuu wa CRDB, Dkt. Charles Kimei amesema kuwa hatua ya Serikali kuhamishia akaunti zake BoT itasaidia kuzuia mfumuko wa bei. Amewataka wananchi wasiwe na hofu juu ya mpango huo, kutokana na hofu iliyojengeka kwamba kuna hatari benki za kibiashara nchini kufilisika. Alisema Serikali ina haki na nia njema kwa kutaka akaunti hizo zifunguliwe BoT kwa kuwa zimekuwa zikifunguliwa kwenye mabenki makubwa ya kibiashara, huku baadhi ya Wakala wa ukusanyaji wa fedha wakishindwa kuzifikisha serikali kama inavyotakiwa. Pia alieleza kuwa mfumo huo hauna utofauti na awali kwani utofauti utakuwepo kutokana na mashirika na taasisi kufungua akaunti BoT, ambapo lengo kubwa ni walaka wa Hazina kulenga kuboresha mapato ya serikali ammbayo yanaweza kutumiwa kwa namna mbalimbali. “Mfumo huu…utakuwa hauna tofauti na ilivyo sasa kwa kuwa fedha zitakazokuwa zikiingizwa kwenye akaunti hizo ni zile zilizokuwa zikiingizwa kwenye benki awali, ili kupunguza kiwango cha riba,” alisema
Sign up here with your email