
Siku mbili baada ya uchaguzi wa uraisi wa FIFA kuisha na Gianni Infantino kuchaguliwa kuwa Raisi wa shirikisho hilo - Mmiliki wa klabu ya Palermo inayoshiriki kwenye ligi kuu ya Italia Serie A, amesema Infatino alishinda uraisi wa FIFA kwa sababu alinunua kura nyingi kuliko mpinzani wake Sheikh Salman. Tuhuma hizo za Zamparini zinakuwa tuhuma za kwanza za rushwa kwa kiongozi huyo wa FIFA, ambaye ni mrithi wa Raisi Sepp Blatter ambaye alijiuzulu kutokana na tuhuma za rushwa zilizokithiri.
Sign up here with your email
