
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye amesema watahakikisha wanakuza mchezo wa ngumi hapa nchini kwa kuwa na ushirikiano wa karibu zaidi na shirikisho la ngumi duniani WBF.
Waziri Nape amesema, katika mkakati wa kukuza mchezo huo hapa nchini amekaa na Rais wa WBF Howard Goiberg ambapo wameongea mambo mbalimbali ambayo yatachangia kukuza mchezo huo ambao ndiyo wa kwanza kuleta medali hapa nchini.
Nape amesema, serikali ya awamu ya tano imekusudia kuwekeza katika michezo mbalimbali tofauti na hapo awali ambapo walikuwa wakiwekeza katika soka pekee ambapo watu wa ngumi wamejitolea kwa ajili ya mafunzo pamoja na ushauri ambao utasaidia kukuza mchezo huu.
Nape amesema, watahakikisha wanaweka uongozi na muundo ambao utaleta nidhamu katika michezo ili kuweza kukuza zaidi michezo na kuendelea kuitangaza nchi kupitia michezo mbalimbali.
Sign up here with your email