Wizara ya Elimu, Sayansi , Teknolojia na Ufundi nchini Tanzania imewasimamisha kazi watumishi watatu wa Taasisi ya Elimu nchini Tanzania TIE kutokana na kushindwa kusimamia vyema zabuni.
Zabuni hiyo ni ile iliyotolewa kwenye moja ya kampuni iliyopewa dhamana ya kuchapisha vitabu vya kujifunzia kwa shule za awali.
Akitoa uamauzi huo katibu mkuu wa Wizara ya Elimu Maimuna Tarishi amesema kuwa viongozi hao wanasimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa makosa ya kuruhusu uzembe huo kufanyika na kufikia hatua ya vitabu hivyo kuletwa wizarani.
Tarishi amesema kuwa wizara yake haitavipokea vitabu hivyo ambavyo hata hivyo makosa yake yanaonesha dhahiri kuwa ni upotezaji wa pesa za serikali na havifai kwa matumizi kwa walengwa.
Sign up here with your email