Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh. Charles Kitwanga wakati alipofika katika makao makuu ya polisi jijini Dar es salaam kutangaza mkakati wa kutokomeza majambazi baada ya tukio la hapo jana la kuuawa kwa askari na raia katika benki ya Accses Mbagala.
Akiongelea juhudi zilizochukuliwa na jeshi la polisi katika kuwakamata majambazi hao kamanda wa jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam Simon Sirro amesema kuwa jeshi limefanikiwa kuwaua majambazi watatu, kuokoa silaha pamoja na kuwakamata wanaotumia vifaa vya polisi kufanyia ujambazi wakijidai wao ni polisi.
Sign up here with your email