HALIMA MDEE AWAKA UCHAGUZI WA MEYA. - Rhevan Media

HALIMA MDEE AWAKA UCHAGUZI WA MEYA.





Mbunge wa Kawe Mhe. Halima Mdee akitoa ufafanuzi nje ya jengo la Jeshi la Polisi Kituo cha Kati mara baada ya Jeshi hilo kuwakamata wanachama watatu walikuwa wameudhuria uchaguzi wa Meya wa Jiji kwa madai kuwa wamesabanisha vurugu.

Madiwani wanaounda umoja wa UKAWA wakiwamzuia Mwenyekiti wa uchaguzi wa Meya wa Jiji mara baada ya kuhairishwa kwa uchaguzi huo kupitia zuio lililotolewa na Mahakamani ya Kisuti tarehe 5/2/2016.
Hapo awali msimamizi wa uchaguzi huo alitaka kupata kujua uhalali wa zuio hilo kutoka Mahakama ya kisutu na mara baada ya mabishano ya takribani masaa mawili baina ya Mwenyekiti wa uchaguzi huo na wanasheria wa CHADEMA, Fred Kihwelo akiongozwa na Halima Mdee walieleza kutokuwa na uhalali wa zuio hilo kwani halikuwa na lengo la kuzuia uchaguzi huu wa tarehe 27/2/2016 na badala yake lililenga kuzuia uchaguzi ulikuwa unatarajiwa kufanyika tarehe 8/2/2016

Na mkurugenzi aliwaita Wajumbe wote wa uchaguzi huo na kusoma orodha ya mahudhurio na kutamaka akidi imefikia pamoja na kufungua kikao huku akiwatambulisha wajumbe wa kikao hicho.
Muda mfupi Kaimu Mkurugenzi alimweleza Mwenyekiti wa uchaguzi huo kuwa amepokea zuio la uchaguzi huo mapema leo asubuhi huku zuio hilo likiwa limebandikwa kwenye lango kuu la kuingilia ukumbini hapo na mara baada ya maelezo hayo Kaimu Mkurugenzi alihairisha kikao hicho.
Mwenyekiti wa uchaguzi alizuiliwa kutoka kwenye ukumbi wa Karimjee mpaka Waziri Tamisemi atakapofi huku polisi wakilazimika kutumia nguvu kumkimbiza.
Na jeshi la polisi liliwakamata wanachama watatu walikuwa wamewasindikiza wabunge na madiwani katika uchaguzi huo na ikawalazimu umati mkubwa ulijitokeza katika ukumbi huo kuelekea kituo cha Polisi cha kati waliposhikiliwa wafuasi hao na kufanikiwa kuwadhamini wanachama wawili na mmoja kubaki kituoni hapo kwa kutoa maelezo zaidi.
Akiongea na wananchi nje ya jengo la Polisi, Mbunge wa Kawe Mhe. Halima Mdee aliwaeleza kuwa wameshafanikiwa kuwadhamini wanachama wawili na mmoja Jeshi la Polisi linamshikilia kwa maelezo zaidi japo kuwa kamanda polisi amewaahidi mpaka ifikapo saa 10 jioni watakuwa wamekamilisha taratibu zote.

Previous
Next Post »