BASATA:MSANII ASIYESAJILIWA HATASHIRIKI TUZO ZA KILI. Baraza la sanaa Tanzania BASATA limetoa tamko kusisitiza kuwa msanii yeyote ambaye hajasajiliwa rasmi na baraza hilo,basi atakua amejiondoa katika nafasi ya kushindanisha Kazi zake kwenye Tuzo za muziki Tanzania (Maarufu Tuzo za kili) Katibu mtendaji wa Barata Godfrey Lebejo amesema kiasi kikubwa cha wasanii wameshajisajili lakini bado wapo ambao hawajafanya hivyo. Usajili unaozungumziwa siyo wa nyimbo au Kazi yoyote ya msanii ila ni usajili wa msanii mwenyewe kutambulika rasmi na baraza na hivyo kushiriki katika Tuzo hizo ambazo pia ni za BASATA
Sign up here with your email