Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano katika sekta ya Mawasiliano Profesa Faustine Kamuzora akizungumza katika uzinduzi wa Safari za ndege za shirika la ndege la nchini Mauritius jijini Dar es Salaam leo. shirika hilo limezindua safari za ndege za kutoka nchini Mauritius kwenda jijini Dar es Salaam na kutoka jijini Dar es Salaam kwenda nchini Mauritius ndege hizo zitaanza safari zake kesho.
Mwenyekiti wa shirika la ndege la nchini Mauritius, Dr. Arjoon Suddhoo akizunumza katika uzinduzi wa safari za shirika la ndege la nchini Mauritius jijini Dar es Salaam leoikiwa na lengo la kuunganisha ushirikiano kati ya nchi za bara la Afrika hasa Tanzania na Nchi ya Mauritius. Safari hizo ni za kutoka nchini Mauritius kuja Dar es Salaam na Dar es Salaam kwenda nchini Mauritius.
Shamlashamla za uzinduzi wa safari za shirika la ndege la nchini Mauritius jijini Dar es Salaam leo.
Sign up here with your email