
TAARIFA KUTOKA YANGA Salamu ndugu zangu, tunaomba kwa wale wote wanaokusanya michango ya kwenda Kigali kwa njia ya magari iwe bus kubwa au bus dogo coaster tunaomba majina na hela ziwe zimewasilishwa pale club jumanne saa tano kamili, kwa ajili ya kuandika barua kwenda ubalozi na wizara ya mambo ya nje kwa ajili ya logistics zingine za mwisho, uongozi hautahusika na safari ambayo uratibu haujafanywa kwa pamoja na uongozi wa club. Imetolewa na mkuu wa idara ya habari na mawasiliano. Jerry C. Muro. 06/03/2016
Sign up here with your email