Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju amesema Rais John Magufuli hana mamlaka ya kikatiba ya kuingilia masuala ya Zanzibar ukiwamo uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika Machi 20.
Hii ni kauli ya pili kutolewa ndani ya wiki moja ikieleza hali hiyo, baada ya ile ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Luvuba aliyoitoa wiki iliyopita baada ya kufanya mazungumzo na Rais Magufuli, Ikulu, Dar es Salaam.
Akizungumza bungeni juzi, Masaju alisema: “Katiba ya Zanzibar si ya Muungano, masuala ya ulinzi na usalama ndiyo ya Muungano na ndiyo sababu ulinzi umeimarishwa visiwani humo kuhakikisha nchi hiyo inakuwa salama
Sign up here with your email