MH TUNDU LISSU AICHACHAFYA SERIKALI. - Rhevan Media

MH TUNDU LISSU AICHACHAFYA SERIKALI.



Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema kutokana na Spika wa Bunge kuteua ‘kiholela’ wajumbe wa kamati za kudumu za Bunge, wabunge wa upinzani hawatashiriki uchaguzi wa wenyeviti wa kamati mbili ambazo zinapaswa kuongozwa na upinzani.
“Kwa mujibu wa mabunge ya jumuiya za madola, kamati hizo mbili lazima ziongozwe na wabunge kutoka upinzani.
Tundu Lissu amedai kuwa katika kamati hizo za Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Mashirika ya Umma (LAAC), wameteuliwa wabunge wa upinzani ambao hawana uwezo mkubwa katika kutekeleza majukumu hayo, “Hili Bunge litakuwa la vichekesho, maana unasema kamati za usimamizi wa fedha za umma zitaongozwa na wapinzani halafu unawachagulia nani aongoze hizo kamati. Hatushiriki uchaguzi acha waendelee.”
Previous
Next Post »