MAN UNITED WAWEKANA KITIMOTO - Rhevan Media

MAN UNITED WAWEKANA KITIMOTO



 KOCHA Louis van Gaal amewaweka kitimoto mastaa wake kwa kuwaita mmoja mmoja ofisini kwake kujieleza kwa nini timu inafanya vibaya.

❖ Van Gaal alikaa kimya kwanza hadi hapo mechi dhidi ya Shrewsburg ilipochezwa na Man United kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 kwenye Kombe la FA Jumatatu iliyopita, ndipo alipoanza kuwaita nyota wote waliocheza kwenye mechi ya kipigo cha2-1 kutoka kwa Midtjylland wiki iliyopita, wajieleze.

❖ Tukio hilo lilifanyika kwenye ofisi yake iliyopo kwenye uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo ya Man United huko Carrington.
Previous
Next Post »