Mchezo
baina ya timu ya Taifa ya Croatia dhidi ya timu ya Taifa ya Ureno
katika michuano ya Uefa Euro 2016, umemalizika kwa timu ya Ureno kusonga
mbele kwa ushindi wa bao 1-0.
Awali
mchezo huo ulimalizika kwa dakika 90 za mchezo kwa kutoka 0-0 na
kuingia hatua ya pili ya lala salama ambazo ziliongezwa dakika 30.
Mchezo huo uliokuwa mkali kwa pande zote mbili, Croatia watajijutia
wenyewe kwa kukosa nafasi nyingi lakini Ureno walitumia nafasi hiyo ya
kipekee na
kuweza
kupachika bao hilo ambalo lilitafutwa kwa taabu na mchezaji nyota wa
timu hiyo, Christian Ronaldo ambaye pia alipiga shuti lake na kuokolewa
na kipa wa Croatia na mpira huo kuja kumpata mchezaji huyo wa Ureno
aliyetokea benchi, Quaresma na kupachika bao hilo kwa kichwa na kufanya
mchezo huo kuwa Croatia 0-1 Ureno.
Mchezaji wa Ureno, Renato Sanches ambaye pia ni mchezaji bora wa mchezo huo akijaribu kumtoka mchezaji wa Crotia
Mchezaji
wa Croatia Perišić’s ambaye alikuwa kivutio kwa mtindo wa nywele zake.
Hata hivyo katika mchezo huo wa leo,licha ya kutegemewa timu yake
imeshindwa kufurukuta na kuambulia kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Ureno
Sign up here with your email